Dmitry Peskov amesema kuwa matamshi ya Jens Stotenberg Katibu Mkuu wa Nato kuhusu vita huko Ukraine yanadhihirisha uwepo wa muungano huo wa kijeshi wa Magharibi katika vita huko Ukraine.
Stoltenberg amesema leo mkutanoni katika
kukaribia kikao cha Mawaziri wa Ulinzi wa Muungano wa Nato huko
Brussels kwamba: ushindi wa Russia katika vita hivyo si pigo kubwa kwa
raia wa Ukraine pekee bali litakuwa pigo na kitendo cha hatari kwetu
sote."
Stoltenberg ameongeza kuwa, Russia imetekeleza mashambulizi dhidi ya miundombinu ya Ukraine na jambo hilo linaonyesha haja ya kutumwa huko Ukraine mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.
Nchi wanachama wa Nato khususan Marekani, Uingereza na Ujerumani zimeingilia vita huko Ukraine kwa kuipatia Ukraine taarifa za kiintelijinsia mbali na kuidhaminia silaha na zana za kijeshi nchi hiyo.